Hong Kong imesema leo kuwa itafunga njia zote za reli zinazoelekea China bara huku Marekani na serikali nyingine zikijitayarisha kuwaondoa raia wake kutoka kwa mji wa China wa Wuhan uliokumbwa na mripuko wa virusi vya Corona ambavyo kufikia sasa vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 100.
Akivalia maski ya kinga , Kiongozi wa Hong Kong Carrie Lam amewaambia wanahabari kwamba huduma za treni zitasitishwa kuanzia saa sita usiku wa Alhamisi na kwamba vituo viwili vinavyounganisha eneo la bara vitafungwa.
Kiongozi huyo alitishia kufunga mpaka kama ilivyofanya Korea Kaskazini na Mongolia lakini akasema kuwa ndege kutoka China bara zitapunguzwa.
Idadi ya waliofariki kutokana na virsui hivyo vipya vya Corona imefikia watu 106 ikiwa ni pamoja na kifo kipya mjini Beijing na vingine 24 katika mkoa wa Hubei ambako visa vya kwanza vilitambuliwa mwezi Desemba.