Wanafunzi 228 wenye mahitaji maalumu wapata kadi za bima ya Afya kwa ajili ya matibabu


Na Rahel Nyabali, Tabora.

Wanafunzi  wenye mahitaji maalumu wapatao 228 kutoka shule ya Furaha na viziwi mkoani Tabora wamepatiwa kadi za Bima  ya Afya ya CHF iliyo boreshwa ambayo itawasaidia kupata matibabu bure bila malipo hatua ambayo itawasaidia wanafunzi hao kuondokana na changamoto ya kupata matibabu kwa wakati.

Akikabidhi kadi hizo za bima ya afya kutoka katika shirika labima ya Afya  CHF  iliyo bolesha  mkuu wa wilaya Komanya Elick amesisitiza jamii pamoja na mashirika mbalimbali mkoani humo kuendelea kutoa msaada kwa watu wasio jiweza hasa wanafunzi ili kuweza kufikia malengo yao.

“Kusaidia watu kama hawa unapata Baraka kwa Mwenyezi mungu niwaombe mashirika binafsi pamoja na wanachi kuwa na moyo wa kuwasaidia wanafunzi hawa tukifanya hivyo taifa letu litazini balikiwa”amesema komanya.

Samwel Elisante mratibu kutoka bima ya afya iliyo boreshwa   CHF amesema kadi hizo zitatumi kwa mda wa mwaka mmoja  wataongezewa mda kila baada ya mwaka kupita.

“Kadi hizi tumezitoa kwa mfumo wa kaya ambapo kaya inatakiwa iwe na watu sita tumefanya na watatibiwa kuanzia ngazi ya zahanati hadi  hospitari ya mkoa”Amesema  Kashonda.

Mkuu wa shule ya ya viziwi   Mgisha Kashonda ametoa shukurani kwa uongozi wa wilaya ya manispaa ya Tabora kwa kuweza kuwawezesha wanafunzi hao kupata kadi za kupata huduma hiyo muhimu

“Tulikuwa tunapata usumbufu mkubwa wanafunzi wakiugua, kwani hapa wanafunzi anatoka mikoa mbalimbali ambapo walikuwa wakipata tatizo mpaka kuwasiliana na wazazi wao hii itatusaidia kuondokana na tatizo hilo’’. Amesema  Kashonda

Aidha Hatua hiyo itawasaidia wanafunzi hao kwa kiasi kikubwa kutokana na baadhi ya wanafunzi kutoka katika mazingira magumu ambao walikuwa wanashidwa kukidhi huduma ya afya licha ya familia nyingine kuwa nje  ya mkoa wa Tabora.