Watumishi wawili wa TRA wafikishwa Mahakamani kwa Rushwa



Na Ezekiel Mtonyole,  Dodoma.

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini TAKUKURU Mkoa Dodoma imewafikisha mahakamani watumishi wawili wa mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Mkoa wa Dodoma kwa kosa la kushawishi na kupokea rushwa ya shilingi milion moja kutoka kwa mfanyabiashara wa jijini  hapa.

Akizungumza na Muungwana Blog ofisini kwake ,  Mkuu wa TAKUKURU  Mkoani Dodoma Sosthenes Kibwengo amesema uchunguzi uliofanywa  na Taasisi hiyo umeonyesha kwamba Jumamosi ambayo ilikuwa Januari  11/2020 majira ya mchana watuhumiwa hao ambao ni  Emmanuel Erenest (31),Vincet Hassan (29),wote wakiwa niwafanyakazi wa TRA, Mkoa wa Dodoma.

Wakiwa katika eneo la majengo jijini hapa,walimkamata mwendesha mkokoteni akiwa na mzigo wa Aluminium kwakosa la kuwa na risiti ya EFD ya tarehe ya nyuma na isiyo na thamani halisi ya mzigo walioukamata.

Ameongeza kuwa " baada ya kuushikilia mzigo huo,walirudi na mwendesha mkokoteni hadi kwenye duka la Maliki Tarimo lililopo maeneo maeneo ya CCM jijini hapa ambapo mzigo huo ulitoka,  na kuacha ujumbe kwa mwenye duka ambaye pia hakuwepo dukani kwake" amesema Kibwengo.

Amesema uchunguzi wa Takukuru unaonyesha kwamba baada ya muda kupita, kwa kuwa waliacha namba kwenye barua ya wito, aliwapigia simu watuhumiwa ambao walimtaka sh milion moja wao wasichukue hatua stahiki.

"Uchunguzi wetu umeonyesha kwamba  watuhumiwa waliacha mzigo walioukamata baada ya kupewa rushwa hiyo na wala suala

hilo hawakulitolea ufafanuzi ofisini kwao,"amesema.

Aidha TAKUKURU inawaasa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kuendelea kutoa taarifa za

vitendo vya rushwa kwa taasisi hiyo ili kuweza kuchukuliwa hatua kwa watu ambao wanaendeleza vitendo hivyo.