Na Paschal Malulu-Kahama
Kufuatia shule ya msingi Mayila iliyopo Kata ya Nyihogo, halmashauri ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga kukabiliwa na uhaba wa madarasa, wazazi na walezi wa mtaa wa Mayila wametakiwa kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa muda wa wiki nne ambapo agizo hilo wamelipinga wakidai hadi kamati ya shule ichaguliwe mpya.
Kauli hiyo ilitolewa jana Januari 29, 2020 katika kikao cha wazazi wa shule hiyo na diwani wa Kata ya Nyihogo kupitia chama cha mapinduzi (CCM), Shadrack Mgwami kuwa wananchi wa mtaa huo wanatakiwa kujenga maboma ya vyumba vya madarasa katika kipindi cha mwezi mmoja ili halmashauri imalizie sehemu inayobaki.
Amesema shule hiyo bado ni mpya na kujengwa kwa shule hiyo ni kutokana na wanafunzi wa mtaa wa Mayila kutembea umbali mrefu kwenda shule hali ambayo ilikuwa ikisababisha wanafunzi wengine kupata ajali ya kugongwa na magari wakati wa kuvuka barabara.
Mgwami amesema shule ya msingi Mayila ina jumla ya vyumba vya madarasa nane ambayo yanatumiwa na wanafunzi wa darasa la awali na la kwanza ambao idadi yao ni wanafunzi 580 hivyo wazazi wanatakiwa kuchangia ujenzi huo haraka ili wanafunzi wa darasa la pili waweze kuhamia na kuepuka kutembea umbali mrefu kwenda shule.
Kwa upande wao wazazi waliohudhuria kikao hicho wamesema kutokana na kamati ya shule kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo hawawezi kuchangia hadi pale watakapochagua viongozi wengine wa kamati ya shule kwani kamati iliyokuwepo imevunjwa.
Mmoja wazazi hao Jumanne Hamis amesema zimekuwepo siasa nyingi katika uongozi wa kamati ya shule kwa kushindwa kusimamia mali za shule ndio maana wamevunja kamati nzima na watakapochagua viongozi wengine ndio watakaosimamia michango ya ujenzi wa madarasa hayo manne.
Ikumbukwe kwenye kikao hicho cha wazazi kiliamua kuvunja kamati yote ya shule kutokana na kushindwa kusimamia majukumu yake na baadhi ya viongozi kutuhumiwa kwa wizi wa mali za shule ikiwemo Saruji, Ndoo za rangi na Vigae huku wazazi hao wakifikia muafaka wa kuchagua viongozi wengine Februari 1,2020.