Babu wa miaka 77 alikuwa akitoa pesa kutoka kwenye mashine ya ukutani. Kibaka wa umri wa makamu alimnyatia na kujaribu kumpora, lakini babu akadinda kuwa mnyonge, akamkunjia ngumi na kurudisha mashambulizi.
Tukio hilo limetokea wales nchini Uingereza majira ya asubuhi ambapo kibaka alikuwa anamnyemelea babu huyo wakati akitoa hela ATM ndipo babu huyo kumshtukia na kuanza kupambana naye ili asiibiwe.