Basi la kampuni ya Premier lagongana na lori na kusababisha vifo


Basi la kampuni ya Premier linalofanya safari zake kati ya Mwanza na Mbeya limegongana uso kwa na lori lenye namba za usajili T486 ANU ambalo lilikuwa likivuta tela lenye namba T 775 APT ambapo limesababisha Vifo vya Watu wawili na majeruhi wanane. Ajali hiyo imetokea asubuhi hii katika kijiji cha Inyala.

Jitihada zinaendelea kwa sasa ni nikuliondoa lori ambalo limeegeshwa barabarani ili kuruhusu magari mengine yaweze kupita.