Bharwani ahoji matengenezo ya gari lake


Na Omary Mngindo, Lugoba

Diwani wa Kata ya Vigwaza Halmashauri ya Chalinze wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani Alhaj Mohsin Bharwani, ameshangazwa kwa hatua ya kutelekezwa gari la kubeba wagonjwa, alilolinunua kwa fedha zake kwa ajili ya kusaidia wananchi ndani ya Kata na Halmashauri kwa ujumla.

Alhaj Bharwani alilihoji Baraza la Madiwani la bajeti ya Halmashauri, ambalo kwa mara ya kwanza likihudhuliwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani Ramadhani Maneno, ambapo Bharwani alitaka taarifa ya matengenezo gari hiyo, aliyoinunua kwa zaidi ya shilingi milioni 45.

Alisema kuwa wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwaka 2015, moja ya ahadi yake ni kununua gari kwa ajili ya kuwasaidia wapigakura wake, ambayo aliitekeleza mwaka 2018 kwa kununua gari aina ya Benzi, kisha kuikabidhi Halmashauri iliyotoa huduma kipindi kifupi, baadae ikaja taarifa kuwa gari hilo limeharibika.

"Ile gari ni nzima nimeinunua kwa zaidi ya shilingi milioni 45 ambazo ningeweza kuzitumia kwa shughuli nyingine, nikaikabidhi Halmashauri lakini kipindi kifupi nikaambiwa imeharibika, nikanunua vifaa ikatengenezwa, nikaambiwa tena inashindwa kufanyakazi, mbaya zaidi kuna kiongozi anawaambiwa wananchi kuwa mashine imewekwa chumvi," alielezea kwa masikitiko Bharwani.

Aidha diwani huyo amesikitishwa na suala la kisiasa kuingizwa katika maslahi mapana ya wananchi, huku akiongeza kwamba kitendo kilichofanywa na kiongozi huyo kinapaswa kulaaniwa, kwani
mbali ya kusababishia hasara aliyeigharamia, pia kinadumaza maendeleo katika eneo husika huku akisema kwamba jambo hilo halifai kufumbiwa macho.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Said Zikatimu aliliambia Baraza hilo kwamba suala la ubovu wa gari hilo wanalo, lakini kuhusiana na uwekwaji wa chumvi kwenye mashine hawana taarifa nalo, huku akimuagiza ofisa anayehusima na usafiri kufanyiakazi suala hilo, kisha kutoa taarifa mapema iwezekanavyo.

Akizungumzia hilo, Ofisa Usafirishaji Jonas Sam alikili kuharibika kwa gari, lakini kuhusu kuwekewa chumvi hana taarifa hiyo na kwamba watalifanyiakazi, huku alisema kuwa halmashauri imelitengeneza sanjali na kulipeleka Wakala wa Matengenezo wa Magari ya Serikali TEMESA, kwa matengenezo lakini bado tatizo katika likionekana kukosa nguvu.

"Diwani Bharwani amewahi kununua vifaa tukalitengeneza, sanjali na kulipeleka TEMESA kwa matengenezo zaidi, lakini kila linapokuwa linawapatia huduma wanaanchi, linaokena kukosa nguvu," alisema Sam.

Akizungumzia suala hilo, Mkurugenzi wa Halmashauri Amina Kiwanuka alisema kuwa wamepokea maelezo ya gari hilo na mengine ya kubeba wagonjwa, huku akiahidi kupitia wataalamu husika kulifanyiakazi na hatima gari i na mengine yaweze kurejea kuwapatia huduma wana-Chalinze.

Akizungumza na madiwani hao, Maneno alianza kusikitishwa kwa taarifa ya kutelekezwa kwa gari hilo lililonunuliwa na mhisani huyo kwa lengo la liwahudumia wananchi, kisha kuhujumiwa jambo alilolielezea halipaswi kufumbiwa macho.

"Uchunguzi wa kina ufanyike kubaini ukweli wa maneno hayo ya kwamba gari hilo limehujumiwa na viongozi, katika maslahi ya wananchi masuala ya siasa zetu tuzizipe nafasi, hili halikubaliki uchunguzi ufanywe kupata ukweli wa hilo jambo," alimalizia Maneno.

Maneno alimalizia kwa kuitaka Halmashauri hiyo wakati ikiwa katika mpango wa kuikarabati gari hiyo wamuandikie barua ya kumshukuru Diwani Bharwani, kwani ameonesha kuguswa na juhudi za serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli ya kuwapunguzia kama si kumaliza changamoto zinazowakabili.