Breaking: Kabendera aachiwa huru


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemwachia huru mwandishi wa habari za Uchunguzi, Erick Kabendera baada ya kulipa faini ya Sh milioni 100 kama adhabu kwa kosa la utakatishaji fedha katika kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa inamkabili, pia ametakiwa kulipa Sh milioni 172 kwa kosa la kushindwa kulipa kodi na Sh milioni 100 au kifungo cha miezi mitatu jela.