Loading...

2/14/2020

DC Sabaya ataja sababu inayorudisha nyumba maendeleo wilaya ya Hai


Mkuu  wa Wilaya ya  Hai, Lengai ole Sabaya, ameeleza moja ya sababu inayochangia kurudisha nyuma maendeleo ya wilaya hiyo ni kutokana na baina ya viongozi kutonia mamoja kwenye utendaji kazi akiwemo  Mbunge  wa jimbo hilo Freeman Mbowe ambapo amemtaka kufanya  maridhiano ndani  ya chama  chake , ndipo  aombe maridhiano na Rais John Pombe  Magufuli.

Hayo yamesemwa na Sabaya leo februari 14,2020, wakati  akikabidhi  pikipiki  17 kwa makatibu  wa kata wa chama cha mapinduzi  CCM wilayani  humo.

Amesema Mbowe  anapokea   fedha za ruzuku   za  chama cha  demokrasia  na maendeleo  (Chadema) zaidi  ya shilingi 360 milioni na kwamba wanachadema  hawajui zinafanyia kazi gani.

Patrick Boisaf ni Mwenyekiti  wa Chama Cha Mapinduzi CCM  Mkoa wa Kilimanjaro ,amesema pikipiki  hizo  zitafanya  Kazi ya chama kwa kurahisisha makatibu  wa kata kuwatembelea wanachama pamoja  na kujua shida  changamoto mbalimbali zinazowakabili.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger