Elimu ya Fedha katika Biashara inatakiwa kuwa hivi

Itakuwa ni bure kama unafanya biashara au unataka kufanya biashara kama utakuwa huifahamu elimu ya fedha.  Elimu ya fedha ndiyo msingi mkubwa wa maisha yako na biashara yako kiujumla.

Elimu ya fedha katika biashara yako inahusika na jinsi ya kupata fedha hizo na jinsi ya kufanya sizipotee.

Elimu ya fedha pia inahusisha masuala mazima kwa ajili ya kujua kile ambacho kinapatikana na kutumika.  Isipojua jinsi ya kupangalia mapato na matumizi yako katika biashara ni sawa bure.

Hivyo ili kuwa mtunza kumbukumbu mzuri katika biashara yako unatakiwa  kuwa na daftari la kumbukumbu ambalo litahusiana na kuweka kumbukumbu zako za kifedha na biashara yako.


Ijue vyema elimu ya fedha ikusaidie kufanikiwa katika biashara yako.

Kwani kuweka kumbukumbu katika daftari kunasaidia kwa kiwango kikubwa kujua kama unapata faida au unapata hasara. Pia kumbukumbu za kibiashara husaidia kuweza kupata taarifa kwa kile kinachoingia na kutoka katika biashara yako.

Lakini nitakuwa sijakutendea haki kama nitashindwa kukueleza ukweli kwamba katika elimu ya fedha lazima ujue ya kwamba fedha inahitaji nidhamu  hasa katika upande wa uwekaji akiba.

Kama umeamua kuitenga fedha kwa ajili ya kuindeshea biashara yako basi jitahidi ubaki katika reli hiyo.

Lakini kama hiyo haitoshi tunashauriwa kwa katika suala la uwekaji akiba ni lazima uwe  kila baada ya muda fulani. Hii ikiwa na maana kama umeamua kutenga kila siku shilingi elfu kumi basi fanya hivyo kwani hii itakusaidia kuweza kuboresha biashara yako pale ambapo itakuwa haifanyi vizuri.

Na wataalamu wa mambo wanasema asilimia 10 ndizo zinatumika kutenga katika uwekaji akiba,  hii inategemeana na kile unachokipata.

Lakini pia pesa yeyote ambayo unapata ni lazima uigawe katika mafungu matano ambayo ni:-

Akiba.

Uwezekaji.

Matumizi ya lazima.

Matumizi yasiyo yalazima.

Fungu la kumi.

Endelea kusoma ukurasa huu kila wakati nitakuelezea kwa undani kuhusu ya ugawaji wa fedha ambazo unazipata,  ila kwa leo tu ni kwambie ya kwamba uhuru wa kifedha katika biashara unahitaji mambo yafutayo:

1. Kufanya kazi kwa bidii.
Kufanya kazi kwa bidii ni siri ambayo ipo katika kupata fedha ambazo unazihitaji.

2. Nidhamu.
Fedha inahitaji nidhamu katika kuipata na namna ambavyo unaweza kuitumia, maana fedha ina makelele mengi, hivyo inahitaji kufanya mambo ya msingi hasa pale inapopatikana.

Mpaka kufikia hapo sina la ziada naomba uyaweke yale niliyokueleza katika matendo maana usipofanya hivyo itakuwa ni sawa na kupika makande kwa mwanga wa mshumaa.

Na; Benson Chonya,