H- Baba aanguka stejini ateguka kiuno

Msanii wa Bongo Fleva H. Baba jana amepata ajali na kuanguka stejini wakati akiingia na swaga zake kwenye Tamasha la “JIPOZE NA TWIST” Mkoani Mbeya.

Baada ya kupata ajali hiyo aliandika ujumbe huu kupitia ukurasa wake wa Instagram: “Jana nimepata ajali jukwani nimetenguka kiuno hii style ni ngumu inaitwa slide nikipona sirudii tena kwa sasa nipo hospital #Asanteni sirudii tena nimekoma ? Slide slide slide sirudii, #Bado nipo hospital kiuno kimeteguka”

H baba alipost picha nyingine akitembea kwa kuchechemea akiwa anaugulia maumivu na kuandika kuwa "hali yangu bado ila mungu anasaidia"