Hazard kukosa mchezo dhidi ya Manchester City


Mchezaji Eden Hazard  wa timu ya Real Madrid ya nchini Hispania,  atakosa mchezo wa siku ya Jumatano wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya dhidi ya Manchester City kutokana na kuwa majeruhi.

Hazard aliumia kifundo cha mguu Jumamosi iliyopita wakati wa mchezo wa Ligi daraja la kwanza Nchini Hispania (La Liga), ambapo Real Madrid ililala kwa kufungwa bao moja kwa bila na Levante.

Hazard mwenye umri wa miaka 29 aliumia katika kipindi cha pili cha mchezo huo na kutolewa uwanjani.

Mchezaji huyo amerejea dimbani siku za hivi karibuni baada ya kukaa nje kwa takribani miezi mitatu akiwa majeruhi.

Hazard, raia wa Ubelgiji ameichezea mara kumi na tano Real Madrid tangu ajiunge na timu hiyo akitokea Chelsea mapema mwaka 2019.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items