Hayo yameelezwa leo Jumatatu Februari 24, 2020 na katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally katika mkutano na waandishi wa habari mjini Dodoma.
Watatu hao waliitwa mbele ya kamati ya maadili ya CCM baada ya sauti zao kuenea katika mitandao ya kijamii zikieleza jinsi CCM inavyopoteza mvuto, uendeshaji wa nchi na jinsi chama kilivyoshindwa kuwalinda makatibu huo dhidi ya mtu anayewachafua.
Membe alifika mbele ya kamati hiyo yenye wajumbe wanne mjini Dodoma baada ya hapo alieleza kufurahishwa na mazungumzo, akisema Mungu alimpa ujasiri wa kuzungumza kile alichotaka kuiambia kamati hiyo na kwamba hakuyumba wala kuyumbishwa katika mahojiano.
Kinana na Makamba walihojiwa na kamati hiyo katika ofisi ndogo za CCM zilizopo mtaa wa Lumumba, jijini Dar es Salaam.
Wengine ambao sauti zao zilisikika katika mkanda huo ni Nape Nnauye, ambaye ni mbunge wa Mtama, William Ngeleja (Sengerema) na January Makamba (Bumbuli) walimuomba radhi Rais John Magufuli.
