Rais wa Marekani Dolnald Trump awasili nchini India


Rais Donald Trump wa Marekani amewasili mjini Ahme dabad, Magharibi mwa India hii leo katika ziara ambayo mataifa hayo mawili India na Marekani yanalenga kuimarisha upya uhusiano wao uliokumbwa mara kadhaa na mvutano wa kibiashara.

 Alipowasili, rais Trump na mkewe walilakiwa na waziri mkuu Narendra Modi ambaye amejenga uhusiano wa kibinafsi na Trump.

 Modi anafanya juhudi zote kufanikisha ziara ya Trump ijapokuwa mkataba wa kibiashara uliokuwa ukishinikizwa na Marekani umeingia matatani.

Serikali ya India imesema nchi yake na Marekani zimejenga uhusiano wa karibu wa kisiasa na kiusalama ambapo ziara hiyo ya siku mbili ya Trump ni ishara ya kuunganisha maslahi yao ya pamoja ikiwa ni pamoja na mbinu za kukabiliana na China kama taifa linaloinukia kuwa na ushawishi mkubwa duniani.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items