https://monetag.com/?ref_id=TTIb Waziri Hasunga awataka vijana kuwekeza kwenye kilimo cha parachichi | Muungwana BLOG

Waziri Hasunga awataka vijana kuwekeza kwenye kilimo cha parachichi

Na Baraka Messa, Songwe.

 Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga amewataka vijana kuitumia vema fulsa ya kuwekeza kwenye zao jipya la parachichi ambalo soko lake ni la uhakika kutokana na uhitaji mkubwa wa matunda ya parachichi katika nchi mbalimbali Duncani.

Akiongea na vijana kutoka mikoa ya Mbeya ,Songwe , Rukwa na Katavi katika ufunguzi wa Kongamano la Vijana kitaifa kushiriki katika fulsa za Kilimo lililofanyika jana wilayani Mbozi Mkoani Songwe alisema Serikali ya awamu ya tano kupitia Wizara ya Kilimo imeamua kujikita kuboresha kilimo kupitia kwa vijana ambao ni asilimia 35 kwa Taifa zima.

Alisema Soko la parachichi ni kubwa Duniani hasa nchi za uarabuni , China na nchi za Ulaya ambapo mikoa ya kusini ina ardhi yenye rutuba ambayo inazalisha zao hilo jipya ambalo pia hustawi vizuri katika mikoa hiyo kutokana na kusheheni ardhi nzuri yenye rutuba, maji ya kutosha kutokana na mito ambayo ina faa katika umwagiliaji msimu wote ili kuzalisha zaidi .

"Vijana wekezeni kwenye kilimo cha matunda hasa parachichi na mboga mboga, serikali ipo tayari kuwatafutia soko nje ya nchi ikiwa mtazalisha kwa wingi kuna nchi nyingi kama nchi za uarabuni hakuna mboga mboga na matunda,
Kuna hela nyingi sana kwenye zao la parachichi wateja ni wengi,  Serikali ipo tayari imejipanga kuleta ndege ikiwa vijana mtazalisha kwa wingi kwa ajili ya kusafirisha kupeleka kwenye Masoko makubwa ndani na nje ya nchi" aliongea Waziri Hasunga.

Aliongeza kuwa Serikali imejipanga pia kuboresha Masoko ya mazao mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutofunga mipaka katika nchi jiran lengo likiwa ni kuhakikisha wakulima wa Tanzania wakinufaika kwa kiasi kikubwa kutokana mazao yao wanayozalisha.

Hasunga vijana kubadilika na kukichukulia kilimo kama kazi ili kuweza kuwekeza katika kulima mazao, kuuza penbejeo, kusindika , kusafirisha mazao ,kuhusika kwenye Masoko na uhifadhi .
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Songwe Nicodemas Meangela alisema asilimia 78 mpaka asilimia 80 ya ya wananchi wanajishughulisha na kilimo katika Mkoa wa Songwe ambapo mkoa umetenga maeneo mbalimbali kwa ajili ya kuwekeza kwenye kilimo .

Alisema Mkoa una hekta bilioni mbili(2) ambazo zinafaa kwa kilimo lakini mpaka sasa ni asilimia 30 tua ambayo inatumika kwa kilimo , hivyo Kuna hekta nyingi ambazo Bado hazijaanza kutumika nchini huku hekta nyingi zikiwa ni hifadhi ya misitu.

"Tayar tumeutangaza mkoa wetu kwa kiasi kikubwa kupitia kongamano la uwekezaji lililofanyika hivi karbuni, hivyo vijana tunawasihi kukimbilia kwenye kazi ya kilimo , Songwe tua soko la uhakika katika nchi mbalimbali zinazo tuzunguka sisi tukiwa kama lango kuu la nvhi za kusini mwa Afrika SADC" aliongea Mkuu wa Mkoa wa Songwe.