https://monetag.com/?ref_id=TTIb Kundi la pili la nzige kuvamia Afrika Mashariki hivi karibuni | Muungwana BLOG

Kundi la pili la nzige kuvamia Afrika Mashariki hivi karibuni


Kundi la pili la uvamizi wa nzige wa jangwani unaweza kulikumba eneo la Afrika Mashariki katika muda wa wiki chache zijazo, wataalamu wa mazingira wameonya. 

Wadudu hao kwa hivi sasa wanataga mayai katika njia yao wanayotumia kupita katika nchi nyingi za Afrika Mashariki, ambayo yatatotolewa katika msimu mwingine wa kupanda mazao na hivyo kuhatarisha kabisa usalama wa chakula. 

Taarifa hizo zimetolewa na Kituo cha Utabiri wa Mazingira na Utendaji (ICPAC) cha Mamlaka ya Ushirikiano na Maendeleo wa Mataifa ya Pembe ya Afrika(IGAD). 

Tahadhari hiyo inakuja baada ya wimbi la mamilioni ya nzige kuvamia Afrika Mashariki katika wiki za hivi karibuni, wakiharibu mazao na maeneo ya malisho katika eneo hilo ambako wengi tayari wanakosa chakula kutokana na ukame na mizozo.