Pompeo awasili Riyadh kwa mazungumzo kuhusu Iran


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo amewasili mjini Riyadh kwa mazungumzo na viongozi wa Saudi Arabia yanayolenga kukabiliana na Iran.

Mwanadiplomasia huyo wa juu wa Marekani ambaye alikuwa ziarani katika nchi kadhaa za Afrika, atafanya mazungumo na Mwanamfalme Mohammed bin Salman sambamba na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia, Faisal bin Farhan.

Ajenda zitakazotawala mazungumzo yake ni pamoja masuala ya kiusalama na kitisho kutoka kwa Iran pamoja na haki za binadamu nchini Saudi Arabia, alisema Pompeo wakati alipozungumza na waandishi wa habari mjini Addis Ababa kabla ya kuelekea Riyadh.

 Ziara yake ya siku tatu kwa mshirika wake wa karibu Saudi Arabia, inakuja baada ya Marekani kumuua kamanda wa ngazi ya juu wa Iran, Qassem Soleimani.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items