Shirikisho la Soka la Morocco limeomba kuandaa fainali za michuano miwili mikubwa ya ngazi ya vilabu barani Afrika ambazo ni Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho.
Morocco inataka mchezo wa fainali ya mabingwa uchezwe kwenye Uwanja wa Mohammed V uliopo jijini Casablana, na mchezo wa kombe la shirikisho uchezwe kwenye uwanja wa Moulay Abdelahh ulioko mjini Rabat.
Ombi hilo la Morocco la kutaka kuandaa fainali hizo za michuano miwili mikubwa limewasilishwa kwa maandishi na shirikisho la soka la nchi hiyo kwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF).