Mashinji uso kwa uso na viongozi wa CHADEMA, Mdee amchunia


Siku chache baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk.Vincent Mashinji kuhamia CCM, leo Feb 24, 2020 amekutana na viongozi wa CHADEMA katika Mahakama ya Kisutu kwenye kesi yao ya uchochezi inayowakabili Mahakamani hapo.

Mashinji amefika akaanza kusalimiana na viongozi mbalimbali wa CHADEMA ambao wapo katika kesi moja akiweno Mbunge Ester Bulaya, John Heche, Peter Msigwa, Esther Matiko na Salum Mwalimu.

Katika hali ambayo haikutarajiwa Mbunge wa Kawe, Halima Mdee ameonekana ni kama amekataa kupeana mkono na Mashinji na kuwa bize na simu yake, pia Mbowe na Mashinji wameonana wakiwa ndani ya chumba cha Mahakama lakini hawakupeana mikono.

Kesi hiyo imeitishwa leo Mahakamani hapa kwa ajili ya kufanya majumuisho ya mwisho kabla ya kutolewa hukumu.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items