Wanawake watakiwa kuwa jasiri katika kugombea nyadhifa za uongozi


Na Timothy Itembe Mara.

Wanawake wilayani Tarime mkoani Mara wametakiwa kuwa jasiri katika swala zima la kugombea nyadhifa mbalimbali za uongozi huku wakiondokana na milapotofu kandamizi zinazomnyima mwanamke kujitokezxa kugombea uongozi  ikiwemo mila ya kuitwa msagane.

Mmoja wa wanawake wilayani Tarime,Ghati Nyerere ambaye ni diwani msitaafu kwenye mkutano wa Mbunge wa jimbo la Tarime,Esther Matiko alisema jana kuwa mwaka huu 2020 ni mwaka wa Uchaguzi kwa hali hiyo wanawake katika majimbo mawili TarimeMjini na Tarime Vijijini Wanawake wanatakiwa kujitokeza kuvuta Fomu za kugombea nafasi mbalimbali ikiwemo Udiwani,Ubunge na hata Urais ndani ya Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema.

Nyerere alisema kuwa Wanawake wameelimishwa vyakutosha juu ya swala zima la kuiitokeza kugombea katika semina mbalimbali kupitia mashirika ya Keserikali pamoja na yale yasiyoya kiserikali kama vile TGNP na mengine mengi  kwahali hiyo hawana sababu ya kuogopa mila kandamizi zilizopo kwa hali hiyo wajitokeze kwa wingi  kugombe anafasi zinazokuwa zimetangazwa kuwaniwa.

Naye Mbunge wa jimbo la Tarime,Esther Matiko aliunga mkono wazo hilo na kuwataka wanawake na wananchi kwa ujumla kumuunga mkono Mbunge huyo mda utakapo wa mchakato wa kugombea na uchaguzi kwa ujumla kwani atajitokeza kutetea nafasi ya ikiti chake pindi itakapotangazwahapo mwezi Okotoba.


"Nasikia baadhi ya watu wengine wanasema kuwa nitateuliwa nafasi ya Ubunge kupitia viti maalumu mimi nasema nitajitokeza kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Tarime nakutetea nafasi ya kiti changu na sitakuja kupitia viti maalumu naamini wanananchi na wanawake wenzangu mtaniunga mkono"alisema Matiko.

Matiko alitumia nafsi hiyo kuwaambia wananchi wa jimbo lake kudhamini mchango wa maendeleo aliotoa ndani ya kipindi cha miaka mitano aliochaguliwa ambapo alisema kwa miaka mitano miundombinu ya barabara imeliomwa na kipaumbele chake kikiwa Elimu.

Kwa upande wake Bashiri Abdala Selemani (Sauti) alisemas kuwa mwaka 2020 ni mwka wa Uchaguzi kwahali hiyo wanwake wajitokeze kwa wingi kugombea wakiwemo kutoka ndani ya Chama chake ili kuondoa urasimu wa mila kandamizi zinazompinga mwanamke kuwa kiongozi.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items