https://monetag.com/?ref_id=TTIb Serikali yaja na mwarobaini wa mimba Mashuleni | Muungwana BLOG

Serikali yaja na mwarobaini wa mimba Mashuleni

KATIKA kukabiliana na utoro na mimba kwa wanafunzi, Serikali imekuja na mikakati kadhaa ya kukabiliana na tatizo hilo ikiwa ni pamoja na ukamilisha mwongozo kwa ajili ya kuimarisha unasii shuleni kuanzia mwaka huu.

Akizungumza na mwandishi wa makala hii, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (anayeshughulikia elimu) , Gerald Mweli alisema baada ya kukamilika kwa mwongozo huo wataanza kutoa mafunzo maalumu kwa walimu wawili kila shule ya jinsi ya kuendesha elimu ya unasii hususani kwa watoto wa kike wanapoanza kupevuka.

“Tumepanga kuanza na walimu wawili kila shule ili kuhakikisha wale watoto sasa wanapatiwa elimu jinsi ya kuepuka vishwawishi na kujilinda ili kuepuka mimba za utotoni na kukatishwa masomo yao.

“Hii programu tunaianzisha makusidi na serikali ya awamu ya tano imeamua kulitekeleza hili kuhakikisha tunapunguza mimba za utotoni na mimba zisizotarajia shuleni na kuhakikisha mtoto wa kike anapoanza shule anamaliza.”

Mweli alisema mkakati wa pili ni ujenzi wa mabweni na kuwa mpaka sasa mabweni yaliyojengwa nchi nzima asilimia 90 ni ya wanafunzi wa kike.

“Tumejenga mabweni mengi sana katika maeneo mbalimbali, na asilimia 90 ya mabweni yaliyojenga ni ya watoto wa kike, kwa kadrili itakavyowezekana Serikali inataka kuhakikisha mtoto wa kike yuko salama, hasa kwenye maeneo ambayo watoto akike wanatemba umbali mrefu.

Mweli alisema lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2025 maeneo yote ambayo ni hatarishi wanafunzi wanapatiwa nafasi ya kuishi shuleni.

“Ndani ya miaka mitatu, tumetumia takribani shilingi bilioni 45 kwa kazi ya ujenzi wa mabweni ya watoto wa kike, sisi kama Serikali malengo yetu ni kuhakikisha mtoto hapi mimba.

Mweli aliongeza: “ hatutaki kuzungumzia suala la mwanafunzi aliyepata mimba kurudi shuleni, hapana Serikali inataka mwanafunzi asipate mimba, kwani tafiti zinasema hata akirudi shuleni anashindwa kuendelea vyema na masomo kutokana na athari za kisaikolojia

“ Serikali hii kwa kuwapenda sana watoto wa kike imesema kwamba mpango wetu ni kwamba hakuna mimba kwa watoto wa kike, na tumefanya hivyo kwani tumetumia zaidi ya shilingi bilioni 45 ndani ya mika mitatu kuhakikisha tunajenga mabweni kwa ajili ya watoto wa kike ili kuwakinga na vishawishi.

“ Pamoja na kuwaepusha na vishawishi kwa kujenga mabweni, lakini pia tumesema tunawajengea uwezo wa kutambua na kukabiliana na changamoto zinazowazunguka, ndio maana tunamalizia mwongozo, utakapokamilika tutato mafunzo kwa walimu ili kuhakikisha watoto hawa wanapata malezi shuleni.

Aidha, Mweli pamoja na kutotoa takwimu alisema kumekuwapo na idadi kubwa ya wanafunzi wakiume wanaocha shule katika ngazi ya elimu ya sekondari ikilinganishwa na wakike.

“ Kwa sekondari takwimu zinaonesha watoto wengi wa kiume wanaocha shule kuliko wakike, awali changamoto kubwa ilikuwa kwa watoto wa kike lakini kwa sekondari inaonesha watoto wakike wanaendelea vizuri kuliko wa kiume.

“ Changamoto kubwa ya watoto wa kiume kuacha shule ni kubwa kwenye maeneo ya migoni kutokana na wengi kujiusisha na kazi za mapema na kutengeneza fedha au maeneo yenye maendeleo makubwa ya viwanda, na tatizo hili si kwa Tanzania pekee.”

Akizungumzia uwiano kati ya wanafunzi wa kike na wakiume wanaoendelea na masomo katika ngazi za juu, Mweli alisema kama nchi hili imekuwa ikifanya vizuri ingawa kumekuwa hakuna mfanano mwaka hadi mwaka.

“Kwa mfano watoto walioacha shule kwa mwaka huu wamepunguza kwa takribani asilimia moja na pointi ukilinganisha na miaka iliyopita.”

“ Mikakati hii itaimarisha zaidi uhudhuriaji wa wanafunzi shule, tunataka mtoto anapoanza shule amalize, kumekuwapo na tofauti dogo kati ya mtoto wa kike na wakiume katika ufualu na uhudhuriaji sisi kwetu ni mafanikio makubwa.”

Mweli alisema kwa sasa kumekuwa na changamoto ya wazazi na walezi kutowasimamia na kuwafuatilia watoto wao kujua kama wanafika shuleni na kusoma.

Alisema tatizo hilo limekuwa kubwa katika mikoa ya pwani na kuwahimiza wazazi kuwa mstari wa mbele kuhakikisha watoto wao wanapata elimu.

“ Hata tukijenga shule nzuri kama mazazi hatakuwa msimamizi wa kwanza wa mwanafuzi, kabla hatujachukua maudhurio suleni, mzazi atajua mtoto wake amelala, na tumekuwa tukipa wasamalia ambao wanatupa taarifa kama wamewaona watoto wanarandaranda kwa shule za serikali na binafasi na sisi tumekuwa tukichukua hatua hatua za haraka.

“ Tunataka mwanajamii akiona wanafunzi aweze kumuuliza mtoto unafanya nini haba baada ya kuwa shuleni? na ikimfahamu ametoka shule gani basi tujulishwe ili tuchukua hatua za kinidhamu za haraka.”

Aidha, Mweli alisema ofisi ya TAMISEMI iko katika hatua ya mwisho ya kuanzisha ‘call center’ kwa ajili ya kupata taarifa mbalimbali itakayofanya kazi kwa saa 16 kwa siku.

“ Kukiwa na taarifa yoyote hata za utoro wa wanafunzi tutataka zitufikie, ikiwa ni suala lolote kero, changamoto, sisi Tamisemi tunataka kuwa karibu sana na wananchi ambao ndio wateja wetu. Hatutaki mwalimu au mzazi asafiri kutoka Ngara kuja Dodoma kuuliza taratibu za kuhamisha mtoto, hivyo tuko katika hatua za mwisho za kufanya hilo.”

Kuhusu nyumba za walimu, Mweli alisema wameshatuma zaidi ya Sh bilioni 9 katika halmashauri ili kukamilisha nyumba za walimu na kupitia mradi wa P4R zaidi ya Sh bilioni 16 zimetumika katika ujenzi wa nyumba za walimu.

“Tunatambua changamoto za walimu ikiwamo ya uhaba wa nyumba, na kwa kutambua hilo ndio maana mwaka huu hatujatoa fedha ya kujenga nyumba yoyote ya watumishi hata kwa wakuu wa wilaya zaidi ya walimu.”