Mawaziri wa ulinzi wa NATO wakutana Brussels

Mawaziri wa ulinzi wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO wanakutana leo mjini Brussels kujadiliana juu ya kuimarisha kikosi chake cha mafunzo nchini Iraq.

Mkutano wa Brussels unafanyika baada ya Marekani kusema kuwa NATO inapaswa kuongeza shughuli zake za kijeshi katika eneo la Mashariki ya Kati.

Kuelekea mkutano huo wa leo, Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg, amesifu mafanikio ya kikosi hicho kwenye kuimarisha uwezo wa vikosi vya jeshi la Iraq katika mapambano dhidi ya kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS.

Stoltenberg amesema jumuiya hiyo inaweza kufanya zaidi nchini Iraq na mawaziri wanaokutana wanaweza kukubaliana kuongeza wanajeshi 200 katika kikosi cha NATO nchini Iraq.

Baadhi ya shughuli za NATO zilisitishwa mnamo mwezi Januari baada ya kuongezeka uhasama kwenye eneo la Ghuba uliochochewa na shambulizi la Marekani lililomuua kamanda wa jeshi la Iran, Qassem Soleimani.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items