Wizara ya mambo ya nje ya Canada imetangaza kuwaondoa raia wake 188 waliokuwa Hubey nchini China .
Waziri wa mambo ya nje wa Canada François-Philippe Champagne amesema kuwa raia 188 wa Canada waliokuwa katika jimbo la Hubey nchini China wamesafirishwa kutoka nchini humo kufuatia janga la virusi vya corona vilivyoikumba China tangu mwishoni mwa mwaka 2019.
Watu zaidi ya 1100 wamekwishafariki kutokana na virusi vya corona aina ya "Covid-19".
Wizara ya mambo ya nje kwa ushirikiano na wizara ya afya nchini Canada vimefahamisha kuwa watu hoa 188 wamepelekwa katika kituo cha afya ambapa watafanyiwa uchunguzi kwa muda wa siku kadhaa.
Kituo hicho cha afya kinamilikiwa na jeshi katika mji wa Trenton Ontario.
Watu wengine 213 waliosafirishwa kutoka Wuhan , uchunguzi wa kiafya utaendelea kwa zaidi ya wiki mbili.
Nchini Canada, ni watu 7 ambao wamepimwa na kukutwa na virusi vya corona.