Njombe: Wafugaji wa samaki washauriwa kupanda samaki msimu wa joto


Na Amiri kilagalila, Njombe

Wafugaji wa samaki mkoani Njombe wameshauriwa kuanza kupanda samaki katika msimu wa joto ili kutoathiri ukuaji wa samaki kutokana na uwepo wa baridi kali kwa baadhi ya msimu ambao husababisha samaki kushindwa kukua kutokana na baridi kali.

Mkoa wa Njombe ni mkoa wenye baridi kali kuanzia mwezi wa tano mpaka mwezi wa nane hivyo hali hiyo imetajwa kuwa inaathiri ufugaji wa samaki mkoani hapa licha ya kuwa wafugaji wengi wa samaki wamehamasika kuanza ufugaji huo.

Grolia Yona ni mtafiti mwandamizi kutoka taasisi ya utafiti wa uvuvi sekta ya kilimo anakiri kuwa baridi ndio sababu kubwa inayofifisha ufugaji wa samaki mkoani Njombe huku akitoa ushauri kwa wafugaji kuanza upandaji wa samaki mwezi wa nane ambao ni msimu wa joto.

“Tunashauri kama mwezi wa nane ikawa ndio wanapanda ili waje waweze kuvuna mwezi wa tano wa sita,na kipindi cha baridi waweze kusafisha mabwawa  yao wajaze maji kwa ajili ya kuanzia mwezi wa nane na watisa wasimame waweke tena samaki”alisema Grolia Yona

Godfrey Kongo ni daktari wa mifugo kutoka halmashauri ya mji wa Njombe amesema halmashauri imeendelea kutoa elimu kwa wafugaji wa samaki ikiwemo namna ya kukabiliana na hali ya baridi ili kuahakikisha uzalishaji wa samaki bora unaongezeka na kuwaletea faida wafugaji.

Pamoja na changamoto mbali mbali baadhi ya wafugaji wamewataka wananchi mkoani humo kuanza kufuga samaki ili kutumia kama vyakula katika maisha yao ya kila siku ikiwa ni mbinu mbadala ya kukabiliana na changamoto ya udumavu mkoani hapa.

“Hata dagaa ni bora sana katika afya ya watoto na katika uchumi inasaidia na maisha yanaendelea mbele,na kwenye samaki unapata vitamin A,huu ni mfugo mzuri na watoto wakila kwa wingi hawawezi kuwa na udumavu”walisema baadhi ya wakulima
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items