Na Adelina Ernest ,Katavi.
Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi Salekhe Muhando amepiga marufuku Mwanafunzi kusitishwa masomo yake kwa kukosa sare ya shule.
Akizungumza na wandishi wa habari amesema kuwa Mwanafunzi hatakiwi kusitishwa masomo Bali walimu wanatakiwa kuwasisitiza wazazi kununua sale hizo huku Mwanafunzi akiendelea na masomo yake
Hata hivyo amewataka wazazi na walezi kuwapeleka shule Mwanafunzi wa kidato cha kwanza na dalasa la kwanza kabla ya tarehe 15/2/2020 kwa atakae kwenda kinyume na tarehe hio hatua za kisheria zitachukuliwa .
Baadhi ya wazazi wilayani humo wamelalamika kuwepo kwa kasumba ya baadhi ya walimu kuwafukuza wanafunzi kwa kutokua na sale ya shule na kumuomba mkuu wa wilaya kushughulikia suala hilo.
