Mpango wa karne wa Trump ni tishio katika ukanda

Rais wa Uturuki asema kuwa mpango wa amani wa karne wa rais wa Marekani ni tishio katika ukanda

Rais wa Uturuki asema kuwa mpango wa amani wa karne wa rais wa Marekani ni tishio katika ukanda.

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp ErdoÄŸan asema kwamba  mpango wa amani ambao rais Trump  amesema kuwa ndio mpango wa karne Mashariki ya Kati ni tishio katika ukanda.

Tunasubiri  shirikisho la ushirikiano wa mataifa ya kiislamu kuandaa mkutano  wa wanachama wake  kwa ajili ya kuonesha  msimamo wa pamoja dhidi ya mpango huo wa rais wa Marekani amesema rais  ErdoÄŸan.

Hayo rais  ErdoÄŸan ameyazungumza  katika mkutano wake na wanahabari  akiwa katika ndege kutoka nchini Pakistani ambapo alikuwa katika ziara yake rasmi.

Katika mkutano wake huo na wanahabari, rais ErdoÄŸan amesema kuwa  kunasubiriwa mkutano wa mataifa ya kiislamu kufanyika ili kuchukuliwa maamuzi ya pamoja dhidi ya mpango huo wa rais wa Marekani kuhusu Mashariki ya Kati.

Mataifa ya Afrika na Umoja wa Ulaya hayakubaliani na mpango huo,  msimamo huo  unaonesha matumaini Umoja wa Mataifa kuhusu mpango wa Trump ameendelea kufahamisha rais ErdoÄŸan.