Msaada wa Qatar kwa Ukanda wa Gazza

Qatar kutoa msaada wenye thamani ya mamilioni ya dola kusaidia kuboresha hali za wakaazi wa ukanda wa Gazza

"Kamisheni ya kuijenga upya Gazza ya Qatar”  imefikia uamuzi wa kutoa msaada wenye thamani ya dola milioni 14 kwa Gazza.

Taarifa ya maandishi iliyotolewa na Hamas ilisema mjumbe wa Hamas alikutana na Rais wa kamisheshi na kujadiliana kuhusu kuboresha hali za raia wa Gazza.

Wawili hao walikubaliana kuhusiana na kuboresha hali za maisha za raia wa ukanda wa Gazza, eneo ambalo linakaliwa kimabavu na walowezi wa kiyahudi.

Katika taarifa hiyo ilisemwa kwamba Qatar itatoa msaada wa dola 100 kwa familia 120 elfu zenye mahitaj. Pia kutakuwepo na msaada wa dola 500 kwa wale watakaohitaji kufunga ndoa.

Qatarpia itajenga upya nymba za wakaazi masikini, Pia kutakuwa na fuko la dola milioni 1 kwa ajili ya kulipia gharama za wanafunzi wa chuo kikuu wanaomaliza masomo yao ili wapatiwe vyeti vyao.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items