Viongozi wa Umoja wa Ulaya washindwa kuelewana kuhusiana na bajeti ya Umoja huo

Viongozi wa mataifa ya Umoja wa Ulaya wamekutana mjini Bruksels kujadiliana kuhusu bajeti na matumizi ya Umoja huo, mpaka mkutano unamalizika muafaka umeshindwa kupatikana

Viongozi wa mataifa 27 ya Umoja wa Ulaya wamekutana mjini Bruksels, Ubelgiji kujadili kuhusu ukubwa wa bajeti na matumizi ya bajeti husika. Katika mkutano huo muafaka haukupatikana.

Rais wa baraza la Umoja wa Ulaya, Charles Michel na rais wa kamisheni ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leven waliongea na wanahabari mara baada ya mkutano huo.

Michel alisema ili muafaka wa bajeti uweze kupatikana muda zaidi ulihitajika. “tumeshindwa kufikia muafaka kuhusiana na bajeti ya Umoja wa Ulaya”.

Von der Leyen  kwa upande wake alisema,

" tumefanya majadiliano marefu na viongozi, tutaendelea na mazungumzo. Ili kuweza kupata matokeo tuna hatua ndefu ya kupiga”.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items