Rais wa Marekani Donald Trump amesema alipitia masaibu makubwa wakati wa mchakato wa kumuondoa madarakani.
Kwenye matamshi yake ya kwanza tangu baraza la seneti kumuondolea mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka, Trump amesema watu ambao walikuwa mafisadi na ambao hawakuwa wakweli walimtia katika hali mbaya zaidi.
Akishiriki mlo wa asubuhi na watu wenye ushawishi mkubwa mjini Washington, Rais Trump amesema, watu ambao hakuwataja majina walifanya kila jambo waliloliweza kuwaangamiza vibaya na hivyo kuidhuru nchi.
Trump amesema atatoa taarifa baadaye leo katika Ikulu na kwamba atajadili kujitolea kwake na kwamba yaliyotokea wakati wa mchakato wa kumtimua madarakani hayawezi kuruhusiwa kuendelea.
Hapo jana, baraza la Seneti la Marekani lilimuondolea hatia Rais Donald Trump kwa kura 52 dhidi ya 48, na kuhitimisha mchakato wa mashtaka dhidi yake, ambamo wabunge wa chama cha Democratic walimtuhumu kutumia vibaya madaraka na kuzuia uchunguzi.