RPC afunguka kuhusu Harmonize kuzuiwa kufanya show Mbeya

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya ametoa ufafanuzi juu ya kuzuiwa kwa show ya mwanamuziki Harmonize ambayo ilifanyika siku ya jana.

"Mimi nina barua ungekuwa karibu ningekuonesha barua waliyonayo, hiyo ingekuwa ya kuziba mdomo, wao waliomba kuwa watafanya show kuanzia Saa 4 Asubuhi mpaka Saa 4 usiku, yeye kaja ukumbini Saa tano Usiku, hapo mkosaji Polisi au mkosaji Harmonize"-RPC Mbeya •

"Pamoja na kuwa Saa 4 ilikuwa ni mwisho, Askari walitumia busara zao za kawaida za kuona Wananchi wamelipa fedha zao kuwazuia itakuwa unfair, wakamwacha aoneshe show kidogo, alichoandika si cha kweli, Wasanii wafuate ratiba, maana kuna suala la Security ya Watu wetu"-RPC Mbeya