Sekondari ya Ndanda yanunua trekta


Na Hamisi Abdulrahmani, Masasi

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashsuri ya Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara, Changwa Mkwazu ameipongeza shule ya Sekondari ya wavulana ya Ndanda iliyoko katika Halmashsuri ya wilayani ya Masasi kwa kuweza kununua trekta  kwa kutumia fedha za mapato ya ndani  ya shule hiyo.

  Ununuzi huo wa Trekta hilo umegharimi  shilingi milioni 53,500,000 ambapo lengo ikiwa ni kuboresha kilimo katika shule hiyo na kujiongezea  mapato.

Mkurugenzi huyo alitoa pongezi hizo  jana kwenye hafla ya fupi ya kupokea na kukabidhi rasmi trekta hilo na kueleza kuwa shule hiyo inapaswa kuigwa na shule zingine.


Alissema ni jambo la fahari kuona shule ikinunua dhana ya za kilimo kama trekta kwa kutumia mapato yake ya ndani.

Mkwazu alisema jambo hilo linapaswa kuwa la mfano kwa shule zingine za halmashauri ya wilaya ya Masasi.

"Huu ni mfano wa kuigwa  kwa shule zingine kwani mmeweza kununua trekta hili kwa fedha zenu za mapato ya ndani na sio mkopo, hivyo mtaongeza mapato ya shule pamoja na kuwafanya wanafunzi kushiriki kazi zingine za maendeleo badala ya elimu ya darasani pekee, hongereni sana" alisema Mkwazu

Akisoma taarifa kwa mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhiwa trekta hilo , Mkuu wa Shule ya Sekondari Ndanda , Morega  Mongate alisema shule ilifikia maamuzi ya kununua trekta hilo kama chombo kitakacho ongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo ukuzingatia shule hiyo ina hekari 60 za kilimo, hivyo litasaidia kulima kwa wakati kuliko kutumia jembe la mkono.

  "Uzalishaji ukiongezeka shule itakuwa na uhakika wa chakula kwa wanafunzi  kwani kuna wakati bei za vyakula inapanda hivyo uzalishaji ukiwa mkubwa ndani ya shule kutakuwa na uhakika wa upatikanaji chakula kwa muda wote shule ni hapa," alisema Mongate

   Mongate alieleza kuwa Shule ya Ndanda inatoa Elimu ya darasani na  ya kujitegemea kwa wanafunzi, ikiwemo ufugaji wa kisasa wa  kuku, Ng'ombe, kilimo na shughuli zingine ili baada ya kumaliza shule waweze kujiajiri na kuajiri kwani shughuli za ujasiliamali ni ajira pia.

    Akiongea kwa niaba ya wanafunzi wenzake,  Simon Kanyasu alisema,  uwepo wa miradi mbalimbali hapo shuleni  ikiwemo mradi wa shamba la shule itawapa uwanja mpana wa kujua kazi mbalimbali.

  Alisema wao kama vijana ambao wanawajibu mkubwa katika kuiletea nchi maendeleo wanafarijika kuona shule hiyo ikilipa kipaumbele suala la kilimo.


Alisema wao licha ya kupata elimu ya darasani lakini wanafaidika kupata elimu kuhusu KILIMO ambapo itasaidia wao kama wanafunzi baadae katika maisha yao.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items