Na Amiri kilagalila-Njombe
Wakala wa misitu Tanzania TFS umejipanga kuimarisha mkakati maalumu wa kupambana na majanga ya moto kwenye misitu ili kupambana na hasara za moto kwenye uwekezaji wa misitu.
Taarifa zinaonyesha kwa kiasi kikubwa swala la majanga ya moto kwenye misitu hususani ya kupanda,inatokana na sababbu mbali mbali ikiwemo kilimo cha kuhama hama na hata shughuli za kibinadamu.
Akizungumza mara baada ya washa ya kukabiliana na moto iliyowakutanisha baadhi ya wadau wa misitu kutoka baadhi ya mikoa ya nyanda za juu kusini Njombe,Iringa na Ruvuma,katika ukumbi wa halmashauri ya mji wa Njombe,ndugu Bakari Mohamed afisa misitu mkuu kwa niaba ya mkurugenzi wa usimamizi wa rasilimali misitu.
Amesema wakulima wanawekeza kwa ghalama kubwa katika kilimo hicho na kupata hasara kubwa na kwa muda mfupi linapotokea janga la moto,hatua inayowalazimu TFS kuunganisha nguvu kati ya serikali,makampuni binafsi,wakulima wakati na wadogo kuwa na mkakati wa pamoja wa kuanzisha kamati kuanzia ngazi ya kijiji mpaka taifa wa kupambana na janga hilo.
“Na wakulima wenyewe wadogo wamefika maala wameona hili ni tatizo kwa hiyo ni swala ambalo ni lazima tuliwekee mkakati maalumu ili tuuunganishe nguvu za pamoja kuanzia ngazi ya chini katika vijiji,kwa hiyo tayari wenzetu wa katika vijiji vya kuzunguka wino mkoani Ruvuma wameshaanzisha kamati za kupambana na moto na tunataka kuchukua kama somo na kuanzisha katika maeneo mengine ya nchi lakini tutaanza na nyanda za juu kusini”alisema Bakari Mohamed
Akitoa mfano wa hasara zinazotokana na janga la moto,amesema TFS kwa mwaka wa jana 2019 ilipatikana hasara ya karibu bilioni mbili zilizotokana na kuungua moto karibu hekta mia sita katika shamba la Sao hili
Jamhuri William ni mkuu wa wilaya ya Mufindi mkoani Iringa ni mmoja wa wajumbe katika washa hiyo,amesema wilaya ya Mufindi inategemea kwa kiasi kikubwa mapato yake na uchumi wa wanachi katika misitu,hivyo swala la moto ni lazima liangaliwe kikamilifu na kuwekewa mikakati ikiwemo kutoa bima katika zaohilo.
“Lakini vile vile kuna swala la bima kwasababu uwekezaji kwenye misitu unatumia fedha nyingi pamoja na rasilimali watu tuone namna gani tunaweza tukahusisha kama taasisi za bima katika kutoa kinga iwapo kutatokea majanga hasa ya moto”alisema Jamhuri Willium
Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri aliyekuwa mgeni rasmi katika washa hiyo,amesema kutokana na faida nyingi zinazotokana na misitu,hivyo ni muhimu halmashauri zinazotegemea mapato yanayotokana na misitu,kuendelea kuwa na sheria ndogo katika kudhibiti moto na kuhakikisha sheria ya misitu na hifadhi inazingatiwa.
“Nitoe wito kwa wote kuhakikisha kwamba sheria iliyopo ya misitu na hifadhi tunaifuta,tuache mazoea sasa hivi miti ni mali sana”alisema Ruth Msafiri
Baadhi ya wadau na wakufunzi katika washa hiyo akiwemo Cherles Ng’asigwa afisa misitu mstaafu amesema ipo haja ya kuanzisha ushirika wa pamoja wa kudhibiti moto utakaosaidi kudhibiti majanga hayo kwa wakati na kupunguza ghalama.
“Nchi za wenzetu pia wamefanikiwa kutokana na ushirika wa kudhibiti moto,ushirika unasaidia kwa kutoa mafunzo lakini pia unapata ratiba ya kuangalia mipaka kiasi ambacho watu wanafanya shughuli kwa pamoja na inakuwa rahisi kudhibiti moto lakini vile vile ghalama zinapungua tofauti na sasa hivi kila mmoja huku kwetu kila mmoja anafanya kivyake sasa ghalama ni kubwa na moto ukianza unasambaa kirahisi sehemu kubwa”alisema Cherles Ng’asigwa
