Serikali imekabidhi vifaa vya kufundishia vilivyotolewa na Canada



Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Serikali imekabidhi vifaa ikiwemo kompyuta 780, komputa mpakato 43 , Printa 74 na vitabu zaidi ya elfu 26 kwa vyuo vya ualimu vya serikali  35 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa kuendeleza elimu ya ualimu Nchini  (TESP) unaofadhiliwa na serikali ya Canada kwa zaidi ya shilingi bilioni 90.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leornad Akwilapo  Akizungumza Jijini Arusha  wakati wa kukabidhi baadhi ya vifaa kwa chuo cha Ualimu Patandi  amewataka Wakuu wa vyuo vyote vya ualimu vya serikali kuvitunza vifaa hivyo ili viweze kuleta tija iliyokususdiwa.

Baadhi ya viongozi na Wanafunzi wa chuo cha ualimu Patandi  Mkoani Arusha wakiwa wamejitokeza kupokea ambavyo Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard  Akwilapo  amevitaja kama nyenzo muhimu katika kuboresha elimu ya ualimu Nchini.


Kansela Mkuu wa ushirikino na Maendeleo kutoka Serikali ya Canada, Gwen Walmsey  amesema hatua hiyo ni ya muhimu katika kuimarisha uwezo wa ufundishaji kwa Waalimu Nchini hivyo kuinua kiwango cha ubora wa elimu nchini.

Mkuu wa chuo cha elimu maalumu patandi Lucian Segla ameishukuru serikali ya Tanzania na Canada kwa utekelezaji wa mradi unaoleta matokeo makubwa katika vyuo vya elimu na kwa taaluma mashuleni kwa ujumla.