Tanesco wataja sababu ya kukatika umeme mara kwa mara wilayani Ludewa


Na Amiri kilagalila,Njombe

Shirika la umeme Tanzania (tanesco) wilaya ya Ludewa mkoani Njombe wamesema sababu ya kukatika kwa umeme mara kwa mara katika wilaya hiyo ni kutokana na udhaifu wa baadhi ya vifaa ambavyo vimefungwa na kuleta changamoto wakati wa mvua zinazoambatana na radi.

Akitoa taarifa ya shirika hilo kwa mkuu wa wilaya ya Ludewa meneja wa tanesco wilaya ya Ludewa Bw,Reubeni Sichone  amesema tayari wameshaomba fedha kwaajili ya kufanya marekebisho maeneo yenye vifaa dhaifu umbali wa kilomita 60.

"Mavundi wako bado wako site licha ya kuwa na udhaifu baadhi ya vijiji hasa kipindi cha mvua zinaponyesha,lakini jitihada zinazofanyika mara baada ya kukatika ni kubadilisha vifaa hivyo,lakini pia tumeomba fedha kwa wahusika na tutafanya matekebisho katika kipande cha kilomita 69" alisema tena Sichone

Katika hatua nyingine Sichone amesema maeneo ya kijiji cha Kingole na kitongoji cha Makale huko tarafa ya Masasi watawashiwa umeme Februari 28 mwaka huu na mkandarasi aliyesaini mkataba wa kazi atakamilisha kazi hiyo April 31 mwaka huu.

"Na ili amalize mkataba wake itakuwa ni kuunganisha wateja na kiekebisha mapungufu" alisema Sichone

Bw,Sichone ametoa wito kwa wananchi kuendelea na maombi ya kuunganishiwa umeme kwa kuwa hata hivyo matarajio ya shirika kwa sasa ni kufungua ofisi ndogo ndogo katika maeneo yao ili ziwe zinatatua changamoto kwa wateja kwa haraka zaidi hasa katika maeneo ya Madindo,Mundindi,Lwilo,na Ntumbati.