Chama cha kihafidhina nchini Ujerumani cha CDU kinachoongozwa na kansela Angela Merkel kitamchagua kiongozi wake mpya wakati wa kongamano maalumu Aprili 25.
Hii ni kwa mujibu wa duru zilizoliarifu shirika la habari la AFP hii leo wakati chama hicho kikijiandaa na hatua ya kuondoka kwa Kansela Merkel.
Chama cha CDU kiliingia katika mzozo baada ya aliyetarajiwa kurithi wadhifa huo Annegret Kramp- Karrenbauer kujiuzulu kama kiongozi wa chama mwezi huu kuhusu kile kinachodhaniwa kuwa kushindwa kwake kuwazuia wabunge wa kikanda kushirikiana na chama cha siasa kali za mrengo wa kulia AFD.
Hatua hiyo ya kushangaza ilifungua mashindano ya kumrithi Merkel ambaye amekuwa uongozini kwa zaidi ya miaka 14 na anayepanga kuondoka madarakani wakati wa uchaguzi mkuu uliopangiwa mwaka ujao.
Kramp-Karrenbauer, anayefahamika kama AKK amefanya mazungumzo na viongozi wa juu wa chama hicho mjini Berlin leo kuamua juu ya kinachofuata.
Duru karibu na mazungumzo hayo, zimeliambia shirika la habari la AFP kwamba wamekubaliana kuandaa kongamano maalumu tarehe 25 mwezi Aprili kumchagua mwenyekiti mpya ambaye atakuwa na uhakika wa kuchaguliwa kuwa mgombea wa chama hicho kuwania ukansela.