Netanyahu atishia kuanzisha vita baada ya Wapalestina kurusha roketi Irsaeli

Wanamgambo katika ukanda wa Gaza waliendeleza mashambulizi kusini mwa Israel leo Jumatatu kwa makombora ya roketi yaliyopenya katika mfumo wa ulinzi wa Israel huku kombora moja likiangukia katika eneo la uwanja wa shule ya chekechea.

Hakuna majeruhi walioripotiwa katika mashambulizi hayo. Hata hivyo mashambulizi hayo yaliyoingia siku yake ya pili yanatishia kuanzisha awamu mpya ya vurugu wiki moja kabla ya Israel kuelekea kwenye uchaguzi.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Nentanyahu aliwaonya viongozi wa kundi la Hamas kuwa iwapo wataanzisha awamu mpya ya mashambulizi basi atafanya mashambulizi ya kulilenga moja kwa moja kundi hilo.

Pande hizo mbili zimekuwa katika vita kati ya mwaka 2008 na 2014. Pande hizo, zilianza tena awamu mpya ya mapigano mwezi Novemba mwaka jana baada ya jeshi la Israeli kumuua kiongozi wa juu wa kundi hilo.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items