Ikulu ya Urusi, Kremlin, leo imeituhumu Uturuki kushindwa kutekeleza makubaliano baina ya pande hizo mbili yaliyoazimia kuzima nguvu za wanamgambo kwenye jimbo la Idlib nchini Syria na kwamba mashambulizi ya makundi ya wanamgambo bado yanaendelea.
Msemaji wa Ikulu ya Kremlin, Dmitry Peskov, amesema Moscow bado inaheshimu mkataba iliyofikia na Uturuki kuhusu Syria, lakini Urusi inayazingatia mashambulizi ya wanamgambo kwenye jimbo la Idlib kuwa ukiukwaji wa mkataba huo.
Maoni ya Urusi yanakuja baada ya Rais Reccep Tayyip Erdogan wa Uturuki kusema jeshi la nchi hiyo litavishambulia vikosi vya jeshi la Syria mahali popote iwapo mwanajeshi mwingine wa Uturuki ataumizwa.
Machafuko yameongezeka kwenye jimbo la Idlib baada ya vikosi vya serikali ya Syria vinavyoungwa mkono na Urusi kupata mafanikio katika kampeni yake ya kuwatokomeza waasi kwenye vita vya miaka tisa vya nchi hiyo.