Rais Xi aahidi kupunguza viwango vya kodi kwa kampuni za biashara

Rais Xi Jinping wa China leo ameahidi kupunguza viwango vya kodi na kutoa msaada mwingine kwa kampuni za biashara wakati serikali yake inajaribu kupunguza taathira za mripuko wa virusi vya Corona kwa uchumi wa taifa.

Taarifa iliyotolewa na shirika la Utangazaji la Taifa imesema hatua hizo zimefikiwa wakati wa kikao cha kamati ya siasa ya Chama cha Kikomunisti cha China, kilichoongozwa na Rais Xi.

Chini ya mageuzi hayo serikali za majimbo zitapaswa kutayarisha mfumo wa kutoa msaada na nafuu nyingine hususani kwa kampuni ndogo na zile zinazomilikiwa na watu binafsi.

Kikao hicho pia kimetoa wito wa kupunguza kiwango cha riba pamoja, kuongeza mtaji wa uwekezaji pamoja na kutoa fedha za kupambana na kudhibiti mripuko wa virusi vya Corona.

Hadi kufikia leo idadi ya waliokufa kwa Corana imefikia watu 1,100 huku visa vya maambukizi vikipanda hadi 44,635 nchini China.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items