Uturuki yafunga mpaka wake na Iran

Uturuki yatangaza kufunga  kwa muda mpaka wake na Iran kutokana na virusi vya corona, Uturuki yatangaza kufunga  kwa muda mpaka wake na Iran kutokana na virusi vya corona.

Uturuki imetangaza kufunga kwa muda mpaka wake na Iran kutokana na  virusi vya corona kuripotiwa nchini humo.

Watu wanane miongoni mwa watu  43 waliopimwa na kukutwa na virusi hivyo wamefariki nchini Iran.

Waziri wa afya wa Uturuki Fahrettin Koca  amefahamisha kuwa atu zaidi ya 80 000 katika mataifa 32  wana virusi hivyo vya corona aina ya Covid-19.

Kufuatia hali hiyo , wizara ya mambo ya ndani na afya zimeafikiana kufunga mipaka na Iran kwa muda.

Waziri wa afya wa Uturuki amesema kuwa raia wanane  wa Iran waliokuwa  na dalili za mafua hawakuruhusiwa kuingia  Uturuki Jumamosi.