Virusi vya Corona vyamuua Daktari aliyegundua mlipuko huo


Daktari mmoja nchini China aliyejaribu kutoa taarifa ya kwanza ya kuwapo mlipuko wa virusi vya corona amekufa kutokana na maambukizo ya virusi hivyo.

Vyombo vya habari vya China vimenukuliwa na BBC vikisema Li Wenliang alikuwa daktari wa macho katika Hospitali ya Wuhan Central, alipobaini na kutuma taarifa ya mlipuko huo kwa madaktari wenzake Desemba 30 mwaka jana.

Baada ya taarifa hiyo, polisi walimwita na kumuonya aache, wakati mamlaka za serikali zilikuwa zikitaka kuzuia taarifa hizo.

Virusi hivyo hadi sasa vimeua watu 560 na kuambukiza wengine 28,000 nchini China.

Daktari huyo alichapisha taarifa yake kwenye mtandao wa Weibo akiwa kitandani, mwezi mmoja baada ya kutoa taarifa za awali za kuwapo kwa virusi hivyo.

Dk Li (34) alikuwa ameona wagonjwa saba wenye maambukizi ya virusi alivyofananisha na ugonjwa wa sars, virusi ambavyo vilitangazwa janga la dharura kwa dunia mwaka 2003.
Mpya zaidi Nzee zaidi