Loading...

Feb 15, 2020

Watanzania punguzeni mahaba na Samatta mtamuharibia kwenye klabu yake- Mwakyembe


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe amesema Watanzania hawana budi kuonesha mapenzi yaliyopitiliza kwa Mtanzania Mbwana Samatta ambaye kwa sasa anakipiga ndani ya Aston Villa ili wasimuharibiwe kwenye Klabu yake mpya na mazoea na wachezaji wenzake.


Waziri Mwakyembe amesema tabia ya Watanzania kuacha kuandika maoni yao yasyokuwa na tija kwa hatna ya Mbwana Samatta.

'Kama unampenda Samatta na umevamia nyumba ya mtu mwingine ishi kama wanavyoishi kama wale, msianze kuleta mambo ya kutukanana, badala yake mnaanza kumgombanisha Samatta na wenzake.' amesema Waziri Mwakyembe

'Niwaombe Watanzania tupunguze mapenzi ya kupitiliza kwa Samatta bali tumuombee' ameongeza Waziri Mwakyembe
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger