Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Azzan Zungu hii leo ameungana na kikundi cha Pamoja Youth katika zoezi la Upandaji miti katika Shule ya Sekondari Buguruni-Moto. Takriban miti 100 imependwa katika eneo hilo ikiwemo miti ya matunda na miti ya vivuli.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Azzan Zungu akiongea na Bw. Stanslav Toldy raia wa Uingereza akiwa ni sehemu ya wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika uzalishaji wa magari yenye kutumia nishati ya umeme. Wawekezaji hao wamemtembelea Waziri Zungu katika Ofisi ndogo ya Makamu wa Rais, Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam.