Daktari afa kwa corona Ufaransa

Ufaransa leo hii imeripoti kifo cha kwanza cha daktari kilichotokana na virusi vya corona.

Waziri wa Afya Olivier Veran amekataa kutoa taarifa zaidi za marehemu kwa kusema, taarifa zake zinahifadhiwa kwa sababu za kitabibu na kuheshimu matakwa ya familio ya dokta huyo.

Daktari alikuwa akifanya kazi katika hospitali ya Compiegne,(Campinyee) huko kaskazini mwa jiji la Paris.

Hosptali hiyo ni kituo cha kwanza kukumbwa na maambukizi. Hadi sasa virusi vya corona vimewauwa watu 562 nchini Ufaransa wengine 6,172 walifikishwa hospitali ambapo robo ya hao wakiwa katika hali mahututi.