Je joto kali linaweza kuuwa virusi vya corona

Baadhi ya watu wanatumai kwamba virusi vya corona vitakuwa hafifu viwango vya joto vitakapopanda, lakini ukweli ni kwamba majanga hayalingani na magonjwa mengine katika kipindi fulani cha mlipuko.

Magonjwa mengi ya maambukizi hutokea wakati tofauti katika mwaka.

Flu ama homa hujitokeza katika miezi ya baridi . Magonjwa mengine kama vile Typhus pia hujitokeza wakati wa msimu wa joto.

Kiwango cha ugonjwa wa surua pia hupungua wakati wa msimu wa joto huku maeneo mengine yakiathirika wakati wa kiangazi.

Watu sasa wanakanganyika iwapo virusi vya ugonjwa wa corona Covid-19 ni hatari zaidi.

Tangu kisa cha kwanza kilipotangazwa nchini China katikati ya mwezi Disemba , ugonjwa huo umesambaa kwa kasi huku visa vingi vikiripotiwa katika bara Ulaya na Marekani.

Baadhi ya mataifa ambayo yameathirika zaidi ni yale yaliopo katika miezi ya baridi, hatua inayozua uvumi kwamba ugonjwa huo utadhoofika na kuwa hafifu kadri mataifa hayo yanapokaribia miezi ya joto.

Lakini wana ukweli kuhusu hilo kwani virusi vinavyosababisha Covid 19 ni vipya na havina ushahidi kwamba vinaweza kubadilika katika mwaka mmoja.

Covid-19 virus, kwa jina Sars, vilisambaa duniani 2003 na vikazuiliwa , ikimaanisha kwamba hakuna data inayojulikana inayoweza kuhusishwa na msimu tofauti kwa mwaka.

Utafiti uliofanywa miaka 10 iliopita na Kate Templeton wa kituo cha magonjwa ya kuambukiza katika chuo kikuu cha Edinburgh , UK ulibaini kwamba aina nyengine tatu ya virusi vya corona vilijitokeza wakati wa baridi na kuendelea kusambaa hadi wakati wa joto.

Virusi hivyo vilionekana kuwa na nguvu kwani vilisambaa kutoka mwezi Disemba hadi mwezi Aprili.

Pia kuna virusi kwa jina Influenza ambavyo pia navyo husababisha virusi vya corona lakini huwaathiri sana wanadamu ambao kinga zao zimedhoofika..

Kuna data chache zinazosema kwamba virusi vya covid 19 vinaweza pia kutofautiana katika mwaka mmoja.

Ukubwa wa mlipuko huu mpya ulimwenguni unaonekana kuwa sawa katika msimu wa baridi na majira ya joto.

Utafiti ambao haujachapishwa kulinganisha hali ya hewa na maeneo kadhaa ulimwenguni, yaliyofikiwa na Covid-19, unaonyesha uhusiano kati ya kuenea kwa virusi na joto, kasi ya hewa na unyevu.

Utafiti mwingine ambao haujachapishwa pia umeonyesha kuwa joto la juu lilihusishwa na kupungua kwa Covid-19, lakini iligunduliwa katika utafiti huo kwamba hali ya joto pekee haikuweza kuzingatiwa kuwa tofauti ya tukio la ugonjwa huu ulimwenguni.

Wakati huo huo, utafiti mwengine ambao haujachapishwa unatabiri kuwa nchi za wastani na zile zilizopo katika eneo la baridi ziko kwenye hatari kubwa kwa athari za Covid-19.

Nchi ambazo ziko karibu na bahari zimetajwa kuwa ndio zilizoathiriwa kidogo, kulingana na watafiti.

Lakini ukweli, ni kwamba magonjwa ya milipuko hayachangiwi na aina tofauti za hali ya hewa.