Malaysia: Jeshi laingizwa mitaani kuimarisha marufuku ya wiki mbili ya watu kutosafiri

Nchini Malaysia leo hii serikali imetawanya jeshi mitaani kuimarisha marufuku ya wiki mbili ya watu kutosafiri katika taifa hilo ambalo lina idadi kubwa ya maambukizi ya virusi katika eneo la Kusini-mashariki mwa Asia.

Mengi mwa maambukizi hayo yanaunganishwa na mikusanyiko ya ibada za kidini. Hadi sasa nchini humo kumeripotiwa vifo tisa na maambukizi 1,183.

Kwa ujumla, eneo la Asia ya Kusini-mashariki limerekodi maambukizi 3,200, ambapo maeneo mengine ni Thailand, Indonesia, Singapore na Ufilipino.

Serikali ya Malaysia imeamua kutumia jeshi baada baadhi ya watu kuendelea kukaidi vizuizi vilivyowekwa Jumatano. Na waziri wa ulinzi kasema utekelezaji wa kijeshi utaanza mchana wa leo.