TPSF na janga la virusi vya Corona

Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) imesema itamfutia uanachama Mwanachama wake yeyote ambaye atalitumia Janga la Ugonjwa wa homa kali ua mapafu unaoenezwa na virusi vya Corona kujinufaisha kwa kupandisha bei ya bidhaa na huduma mbalimbali za kujikinga na maradhi hayo.

Akizungumza jijini Dar es salaa na Waandishi wa Habari,Mwenyekiti wa (TPSF) Angelina Ngaruka amesema Taasisi ya Sekta Binafsi imesikitishwa na vitendo vya baadhi ya wafanyabishara kutumia janga la Ugonjwa huo kuumiza Watanzania kwa kuwapandishia bei mahitaji muhimu ya kila siku ikiwemo dawa na Vyakula.

Aidha, Mwenyekiti huyo amesisitiza kwamba Sekta Binafsi imejiandaa kushirikiana na Serikali kupambana na Ugonjwa wa COVID-19 na athari zake kijamii na kiuchumi na kwamba wameunda kamati maalumu itakayoshughulikia masuala yanayohusu ugonjwa huo.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items