Waliokiuka maagizo ya Museveni ya kukaa karantini wapigwa risasi na polisi


Watu wawili wamelazwa Hospitali Uganda baada ya kupigwa risasi na Polisi kwa kukiuka agizo la Rais Museveni,Alex Olyem na Kasim Ssebude wamepigwa risasi wakati wamepakizana kwenye Bodaboda ambazo zimepigwa marufuku ili kuzuia corona kuenea, mmoja amepigwa tumboni na mwingine mguuni.

“Alex na Kasim wamepigwa risasi kwa kubishana na askari, wanadai hawakufuatilia vyombo vya habari eti marufuku ya Bodaboda kupakiza abiria hawajaisikia, mwanzoni risasi zilipigwa juu wakawa wanakimbia zikapigwa tena mmoja ikampata mguuni mwingine tumboni, wamelazwa”-POLISI UGANDA
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia