Mke na mume mbaroni kwa kusambaza taarifa za uongo kuhusu corona

Polisi kutoa maelezo kumshikilia ofisa LHRC - Mwananchi

Polisi wanawashikilia watuhumiwa wawili Boniphace Mwita na Mkewe Rosemary wakazi wa Tabata, DSM kwa kusambaza taarifa za uongo kuhusu corona wakiwa kwenye daladala ambapo walianza kupotosha, kukejeli na kutania kwa kusema Serikali inapotosha Wananchi kwamba kuna corona”-Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum DSM

“Mwita na Mkewe tunawashikilia kwakuwa wakiwa kwenye daladala walisema Serikali haina fedha kwa ajili ya kulisha wanafunzi ndio maana mashule na vyuo vimefungwa kwa kisingizio cha corona na wakadai Serikali inafanya hivyo ili kuomba msada kwa Mataifa mbalimbali”- MAMBOSASA

Watuhumiwa hao ni :-

1.BONIFACE  ELIAS MWITA (49),Mkazi wa Tabata 

2.ROSEMARY ELIAS MWITA(41)Mkazi wa Tabata ,Mke wa Boniface.

“Baada ya Mwita na Mkewe kusema Serikali inapotosha kuhusu corona na haina fedha ndio maana imefunga shule na vyuo kwa kisingizio cha corona, abiria ktk daladala iliwakera wakawaweka chini ya ulinzi wakamuamuru Dereva apeleke gari Polisi, tunao, tutawapeleka Mahakamani”-MAMBOSASA

MKE NA MUME MBARONI KWA KUSAMBAZA TAARIFA ZA UONGO KUHUSU UGONJWA