Watu zaidi ya 11000 wamekwishafariki kutokana na virusi vya corona wamekwishafariki na kesi 270 000 ulimwenguni.
Watu 11000 wameripotiwa kufariki ulimwenguni na kesi 270 000 tangu kuzuka kwa janga la virusi vya corona katika jimbo la Wuhan nchini China.
Italia ndio taifa barani Ulaya na ulimwenguni lililoathirika kwa kiasi kikubwa na virusi hivyo hatari.
Watu wasiopungua 627 wamefariki nchini humo na kufanya idadi ya watu waliofariki kuzidi kuongezeka na kufikia watu 4032.
Kulingana na vyanzo vya habari kutokana nchini Italia, serikali imetangaza kuchukuwa hatua ya kupiga marufuku kutoka nje.
Wanajeshi na maafisa walinda usalama watuhusika na utekelezwaji wa hatua hiyo.
Nchini Uhispania idadi ya watu ambao wamekwishafariki imefikia watu 1002 baada ya watu wengine 235 kufariki katika muda wa masaa 235.
Mkoani Nice nchini Ufaransa mafuruku ya kutoka nje imetanzwa kuanzia Ijumaa.
Watu 210 wamekwishafariki nchini Marekani , hatua y a kufunga vituo vyote vya biashara mjini New YORK imetangazwa.