Jeshi la Polisi mkoani Tabora linawashikilia watu sita kwa tuhuma za mauaji ya askari wa Jeshi la Wananchi JWTZ aliyefahamika kwa jina Samwel Machugu ambaye anadaiwa kuuawa kwa kushambuliwa na kundi la Vijana wakati alipokuwa akishiriki Ulinzi Shirikishi kwenye mtaa wake kata ya Ipuli eneo la Kidatu katika Manispaa ya Tabora.
Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora ACP Laurian Albert anabainisha kuwa kukamatwa kwa watu hao sita ni matokeo ya Msako mkali unaoendelea kufanyika mjini Tabora ambapo watafikishwa mahakamani muda wowote kutoka sasa.
Aidha katika msako huo Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata silaha bunduki 21 zinazomilikiwa isivyo halali huku nyingine zikidaiwa kutumika katika matukio ya uhalifu.